Wachezaji wa Uganda wapewa hifadhi Uingereza

Kizza Pariyo Haki miliki ya picha Matthew Horwood
Image caption Kizza na Pariyo walienda Uingereza 2014

Wachezaji wawili wa raga kutoka Uingereza walioomba hifadhi baada yao kukataa kurejea Uganda wamekubaliwa kuishi nchini humo.

Wawili hao, Benon Kizza na Philip Pariyo, walikuwa wameenda kushiriki michezo ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow 2014 lakini wakakataa kurejea makwao.

Kwa mujibu wa gazeti la South Wales Evening Post, wawili hao sasa wameruhuwa kukaa nchini humo.

Wanachezea klabu ndogo ya rafa eneo la Cardiff rugby, St Peters.

Mwenyekiti wa klabu hiyo Joe Sweeney ameambia gazeti hilo: "Wote wawili wanafanya kazi sasa.

"Philip anafanya kazi ya kuosha magari naye Benon anafanya kazi ya ujenzi."

Haijabainika ni sababu gani zilitumiwa kuwapa hifadhi.