Terry: Sina mawasiliano na timu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption John Terry

John Terry amesema hajafanya mazungumzo na Chelsea kuhusu mkataba licha ya kocha Guus Hiddink, kusema huenda mchezaji huyo akabaki katika kikosi hicho.

Wiki iliyopita mchezaji huyu alieleza hajapewa ofa mpya huku mkataba wake ukiwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu. Mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi dhidi ya Manchester united, amesema "nimeweka wazi nataka kubaki hapa, japo ni ngumu timu ndio kitu muhimu zaidi na hakuna mawasiliano kati yangu na timu kwa sasa.

Terry alijiunga na timu ya vijana ya Chelsea mwaka 1995, amecheza jumla ya michezo 478 ya ligi kuu ya England. Na kumekua na tetesi anaweza kwenda nchini Qatar katika timu ya Al Arabi, kungana na mchezaji mwenzake wa zamani Gianfranco Zola, ambae ni kocha wa kikosi hicho.