Yanga yaongoza ligi Tanzania

Image caption Watoto wa Jangwani

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania timu ya Yanga imeendelea kuongoza ligi baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Ruvu. Mabao ya Yanga yalifungwa na Simon Msuva aliyefunga mawili na nyingine yakifungwa na kupitia Issofou Boubacar na Donald Ngoma.

Wekundu wa msimbazi Simba wakicheza ugenini ilichapa Kagera Sugar kwa Bao la Ibrahim Ajib, huku mshambuliaji huyu akikosa mkwaju wa penati. Katika dimba la Chamazi Complex, wenyeji Azam FC iliitungua Mwadui FC bao 1-0 kwa goli la mshambuliaji Kipre Tchetche.

Na huko mkoani Mbeya ndugu wawili Tanzania Prison walitoshana nguvu kwa kwenda sare ya 0-0 na Mbeya City. Majimaji ikachomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mgambo JKT.Wakata miwa wa Mtibwa Sugar wakicheza katika uwanja wao wa Manugu huko Turiani Morogoro walikubali sare ya bao 1-1 na Ndanda Fc.

Yanga wanaendelea kukaa kileleni mwa ligi wakiwa na Pointi 43 kwa Mechi 18 wakifuatiwa na Simba wenye na Pointi 42 kwa Mechi 18 huku Azam FC ikiwa na Pointi 42 kwa Mechi 16.