Nusu ya mataifa ya Afrika yakana mgombea wa CAF

Image caption Rais wa shirikisho la Liberia,Musa Bility

Nusu ya mataifa ya Afrika hayaungi mkono mgombea wa Sheikh Salman anayeungwa mkono na shirikisho la kandanda la Afrika CAF.

Mwenyekiti wa shirikisho la kandanda nchini Liberia Musa Bility ameiambia BBC.

CAF ilitangaza ijumaa kuwa inaunga mkono raia huyo wa Bahraini mkono kinyume na matarajio ya wajumbe wengi waliokuwa wameahidi kusimama nyuma ya mgombea wa pekee wa Afrika Tokyo Sexwale kutoka Afrika Kusini.

''Nimezungumza na marais 26 wa mashirikisho ya kandanda barani Afrika na wote wamenihakikishia kuwa hawatamuunga mkono Sheikh Salman'' alisema Musa Bility

Bara la Afrika linajumla ya wapiga kura 54 katika shirikisho la soka duniani FIFA lenye wajumbe 209.

Hata hivyo CAF hainauwezo wa kupiga kura yenyewe kwa niaba ya wanachama wake kwa hivyo kila mwanachama anauwezo wa kupiga kura kwa siri.

Haki miliki ya picha no credit
Image caption Nusu ya mataifa ya Afrika yakana mgombea wa CAF

Katika taarifa hiyo Bility ameitaka CAF iunganishe mataifa ya Afrika kwa manufaa ya kandanda ya Afrika katika utawala ujao utakaorithi kiti kilichoachwa wazi na na kupigwa marufuku kwa rais wa shirikisho hilo

Sepp Blatter.

Licha ya kukosa uungwaji mkono wa CAF mwakilishi wa pekee katika kinyang'anyiro cha urais , Sexwale ameiambia BBC kuwa hatajiondoa katika uchaguzi huo utakaofanyika baadaye mwezoi huu.

Katika uchaguzi wa mwisho uliopita, mwanamfalme Ali ndiye aliyeshindana na Sepp Blatter na akazoa kura 73- 133.

CAF ilitia sahihi makubaliano na kiongozi wa shirikisho la bara Asia Sheikh Salman kujwa watamuunga mkono huku akiahidi kuipa bara la Afrika kipaombele iwapo atachaguliwa.