Shabiki kushinda £25,000 Leicester ikishinda ligi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mashabiki wa Leicester

Shabiki mmoja wa kilabu ya Leicester huenda akajishindia pauni 25,000 iwapo timu yake katika ligi ya Uingereza itashinda taji la ligi hiyo baada ya kuweka pauni tano katika dau la 5,000-1.

Ushindi wa Leicester wa 3-1 katika kilabu ya Manchester City unawaacha wakiwa pointi tano juu ya jedwali hilo huku ikiwa thuluthi mbili za msimu huo zimekamilika.

Carpenter Leigh Herbert, mwenye umri wa miaka 38 alicheza dau akiwa katika likizo na amekataa ombi la kumtaka achukue pauni 3,200 ili kujiondoa.

Iwapo Leicester ambao walikuwa chini ya jedwali la ligi hiyo mwaka mmoja uliopita watashinda taji hilo la ligi,inaaminika kuwa hiyo itakuwa zawadi kubwa kuwahi kutolewa katika historia ya michezo.