West Brom yatinga raundi ya tano FA

Timu ya soka ya West bromwich Albion imesonga mbele kwenye raundi ya tano baada ya ushindi wa penati 4-3 dhidi ya Peterborough.

Dakika tisini zilimalizika kwa timu hizi kwenda sare ya bao 1-1 ambapo Jon Taylor alianza kuifungia timu yake bao la kuongoza kwenye dakika 55, ya mchezo.

Kiungo wa West Brom Darren Fletcher akachomoa bao hilo katika dakika ya 71 ya mchezo huo.

Katika changamoto za mikwaju ya penati wachezaji wa Peterborough Martin Samuelsen na Lee Angol walikosa penati zao.