Abou Diaby kurudi uwanjani baada ya miezi 17 ya jeraha

Haki miliki ya picha PA
Image caption Abou Diaby

Je, unamkumbuka Abou Diaby? Mchezaji wa zamani wa Arsenal? Kila mara akiuguza jereha? Sasa amerudi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anatarajiwa kurudi akiichezea Marsaile baada ya miezi 17 ya kuuguza jereha.

Diaby ambaye aliweza kucheza mechi mbili katika msimu wake wa mwisho na kilabu ya Arsenal aliachwa na kilabu hiyo katika msimu wa joto.

Bahati yake mbaya imeendelea katika taifa lake la Ufaransa baada kupata jereha akiwa zoezini, lakini sasa anatarajiwa kurudi katika mechi ya kombe la Ufaransa dhidi ya Trelissac siku ya Alhamisi.