Sunderland yavunja mkataba na Johnson

Haki miliki ya picha Getty

Klabu ya Sunderland imefuta Mkataba na Mchezaji wake Adam Johnson mara tu baada ya mchezaji huyo kukiri Makosa Mawili Mahakamani kwenye Kesi iliyomkabili ya kuwa na uhusiano wa ngono na Binti wa chini ya Miaka 16.

Johnson, mwenye umri wa miaka 28, aliishtua timu yake baada ya kukiri Kosa moja Mahakamani katika Kesi yake tofauti na kile walichotegemea ambapo sasa amekubali kumrubuni Binti wa Miaka 15 na kumbusu lakini kukana kufanya nae ngono.

Meneja wa Sunderland, Sam Allardyce, alithibitisha kuwa Johnson hatakuwemo kwenye Kikosi cha Timu yao ambacho Jumamosi kitacheza na Manchester United.

Haki miliki ya picha Getty

Mkataba wa winga huyu umevunjwa mara tu baada ya Kampuni ya Kutengeneza Vifaa vya Michezo, Adidas, kuamua kuvunja Mkataba wa Udhamini na Mchezaji huyo.

Kesi ya Johnson itaendelea Bradford Crown Court Ijumaa ambako anakabiliwa na Jumla ya Mashitaka Manne ambayo yote awali aliyakana.

Kwa makosa ambayo ameyakiri, Mchezaji huyo sasa ana hatari ya kufungwa si zaidi ya Miaka Miwili na Nusu.

Johnson, alizaliwa mjini Sunderland alianza kucheza soka katika timu ya Middlesbrough kisha akajiunga na Manchester City kabla ya kusajiliwa na Sunderland, kwa dau la pauni milioni 10 mwaka 2012.