Aubameyang aifungia Dortmund bao la 30 msimu huu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Aubameyang aifungia Dortmund bao la 30 msimu huu

Mchezaji bora bara Afrika mwaka huu kulingana na CAF, Pierre-Emerick Aubameyang aliweka rekodi kwa kufunga bao lake la 30 msimu huu alipoisaidia timu yake Borussia Dortmund kufuzu kwa nusu fainali ya kombe la Ujerumani baada ya kuichapa VfB Stuttgart mabao 3-1.

Raia huyo wa Gabon Aubameyang pamoja na mshambulizi mwenza Marco Reus, wameisaidia klabu yao ya Dortmund kuzoa mabao 45 msimu huu na hawakulegeza kamba walipofunga bao moja kila mmoja naye Henrik Mkhitaryan akaihakikishia Dortmund alama zote tatu.

Kufuatia ushindi huo Aubameyang ameifungia Dortmund katika mechi zote za kuwania kombe la Ujerumani.

"Auba anajua kupima upinzani na kufunga wakati muhimu zaidi naamini kazi yake inaonekana kila siku aingiapo uwanjani''alisema mshambulizi mwenza Reus.

Haki miliki ya picha
Image caption Mchezaji bora bara Afrika mwaka huu kulingana na CAF, Pierre-Emerick Aubameyang

Dortmund walifuzu kwa nusu fainali yao ya tatu mfululizo kufuatia kichapo hicho huko Stuttgart ambayo haikuwa imeshindwa katika mashindano yote tangu mwezi desemba ikipoteza mechi yao ya kwanza.

Timu anayoifunza kocha mpya wa Manchester City,Pep Guardiola, Bayern Munich itakuwa mbioni kujiunga na Dortmund katika nne bora itakapopepetana na VfL Bochum .

Aidha Heidenheim inaialika Hertha Berlin katika mechi ile nyengine.