Payet asaini mkataba mpya

Haki miliki ya picha AFP

Kiungo mshambuliaji wa timu ya soka ya West ham, Dimitri Payet amesani mkataba mpya wa miaka mitano na timu yake.

Payet mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na Wagonga nyundo hao wa London msimu uliopita akitokea timu Marseille kwa dau la zaidi ya pauni milioni 10.

Mapema wiki hii klabu yake ilizikataa taarifa zilizosambaa kuwa mchezaji huyo anataka mkataba mpya, huku mkataba wake wa kwanza pia ukiwa ni miaka mitano.

Mchezaji huyu wa kimataifa wa Ufaransa amezifumania nyavu mara 6 katika michezo 22 aliyocheza na kuiweka West Ham katika nafasi ya sita ya msimamo wa ligi kuu ya England.

David Sullivan, mmiliki wa timu hiyo amesema "tutafanya chochote kuwabakiwa wachezaji wetu wazuri na Payet ni mchezaji mzuri."