Arsenal dhidi ya Leicester, Man City na Tottenham

Leicester Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Leicester kwa sasa wanaongoza ligini

Mechi zitakazochezwa Jumapili baina ya timu 4 za kwanza zitaamua mwelekeo halisi wa ligi hii yenye wapenzi wengi duniani, Ligi Kuu ya Uingereza.

Arsenal itamenyana na Leicester City ambayo bado inaongoza ligi ikiizidi Arsenal alama 5.

Arsenal imo kwenye nafasi ya tatu na ushindi wake utapunguza pengo baina yake na Leicester na kuipa matumaini zaidi ya kuendelea kupigana hadi mwisho.

Nayo Manchester City yenye nafasi ya 4 itaialika Tottenham iliyo kwenye nafasi ya pili.

Bila shaka mshindi atajiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea na mbio za kuwania ubingwa.

Miongoni mwa mechi zitakazopigwa jumamosi hii ni Sunderland kupepetana na Manchester United na Everton kuzipiga na West Brom.

Ratiba kamili na kama ifuatavyo (Saa za Afrika Mashariki

Jumamosi tarehe 13 Februari:

  • Sunderland v Man Utd 15:45
  • Bournemouth v Stoke 18:00
  • Crystal Palace v Watford 18:00
  • Everton v West Brom 18:00
  • Norwich v West Ham 18:00
  • Swansea v Southampton 18:00
  • Chelsea v Newcastle 20:30

Jumapili tarehe 14 Februari

  • Arsenal v Leicester 15:00
  • Aston Villa v Liverpool 17:05
  • Man City v Tottenham 19:15