Arsenal 2 - 1 Leicester

Haki miliki ya picha PA
Image caption Danni Welbeck

Danni Welbeck ambaye alikuwa anacheza mechi yake ya kwanza tangu Aprili mwaka uliopita ameifungia Arsenal bao la pili na la ushindi dhidi ya vinara wa ligi kuu ya Uingereza Leicester.

Welbeck alimhakikishia Wenger ushindi huo muhimu uliotamatisha msururu wa mechi 16 bila kushindwa wa kocha Claudio Ranieri.

Mchezaji mwengine wa akiba Theo Walcot ndiye aliyekuwa ameisawazishia Arsenal kunako dakika ya 70 ya kipindi cha pili.

Wageni hao ambao wamewatamausha wengi msimu huu kwa kufungua pengo la alama 4 kileleni mwa jedwali la ligi kuu ya Uingereza walikuwa wamefunga bao la kwanza kupitia kwa mkwaju wa penalti.

Bao hilo lilitiwa kimiani na Jamie Vardy kunako dakika ya 45''.

Mpira umeisha.

GOOOOOOOL

90'Arsenal 2-1 Leicester

Danni Welbeck anaifungia Arsenal bao la pili

90'Arsenal 1-1 Leicester

Dakika nne za ziada zimeongezwa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Aaron Ramsey (Arsenal) naye anapoteza nafasi nzuri

89' Aaron Ramsey (Arsenal) naye anapoteza nafasi nzuri baada ya kupiga nje pasi ya Alexis Sanchez

Olivier Giroud (Arsenal) anagonga pasi hafifu kipa wa Leicester anaudaka bila wasiwasi

87'Arsenal 1-1 Leicester

Per Mertesacker (Arsenal) anakosa nafasi nzuri mkwaju wa kichwa unatoka nje

85'Arsenal 1-1 Leicester

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Danny Welbeck

Alex Oxlade-Chamberlain anaondoka Danny Welbeck anaingia

Kocha Arsene wenge anamrejesha Danny Welbeck kwa mara ya kwanza tangu mwaka jana alipojeruhiwa

80'Arsenal 1-1 Leicester

77' N'Golo Kanté (Leicester City) anajaribu kutesa mabeki wa Arsenal lakini bila mafanikio

80' Aaron Ramsey (Arsenal) anafyatua kombora lakini wapi

76' Alexis Sánchez (Arsenal) anakosa mkwaju mzuri kutoka kwa Ozil

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Alexis Sánchez (Arsenal) anakosa mkwaju mzuri kutoka kwa Ozil

75'Arsenal 1-1 Leicester

Foul kuelekea lango la Leicester

Aaron Ramsey (Arsenal).

70' Arsenal 1-1 Leicester

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Theo Walcot anaisawazishia Arsenal

GOOOOOOOOL

Theo Walcot anaisawazishia Arsenal

68' Arsenal 0-1 Leicester

Alexis Sánchez (Arsenal) anaongoza mashambulizi mbele ya lango la Leicester lakini wapi.

Mesut Özil naye anasaidia kufyatua makombora lakini safu ya ulinzi ya Leicester imeimarishwa Marcin Wasilewski

65' Arsenal 0-1 Leicester

Theo walcott anaingia uwanjani kuchukua nafasi ya Francis Coquelin.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Theo walcott anaingia uwanjani

Danny Simpson aoneshwa kadi Nyekundu dakika mbili tu baada ya kurambishwa kadi ya njano ya kumchezea visivyo Olivier Giroud

Image caption Arsene Wenger

51' Arsenal wanashambulia lango la Leicester

Olivier Giroud anagonga nje mpira wa kichwa

50' Arsenal 0-1 Leicester

Refarii Martin Atkinson anamuonesha Danny Simpson (Leicester City) kadi ya njano kwa kumwangusha Alexis Sanchez

Image caption Jamie Vardy aifungia Leicester
47' Arsenal 0-1 Leicester

Mesut Özil (Arsenal) anashambulia lakini wapi.

Olivier Giroud amekosa makali mbele ya lango inakuwa ni Golkick.

46' Kipindi cha pili kimeanza .

Jamie Vardy aifungia Leicester bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jamie Vardy ameifungia Leicester

Na kipindi cha kwanza kimekamilika Foxes ama vijana wa Claudio Ranieri wanaenda mapumzikoni wakiongoza kwa bao muhimu dhidi ya washika bunduki wa Arsenal uwanjani Emirati.

Penalti

45 Arsenal 0-1 Leicester

Gooooooool!

Arsenal 0, Leicester City 1. Jamie Vardy (Leicester City)

Nacho Monreal (Arsenal)anaoneshwa kadi ya njano.

Image caption Sanchez

Arsenal waadhibiwa kwa penalti

39' Arsenal 0-0 Leicester

Francis Coquelin (Arsenal) anaoneshwa kadi ya njano kwa kucheza visivyo.

35' Arsenal 0-0 Leicester

Image caption Kocha Claudio Ranieri

Ikiwa matokeo yatasalia hivi hivi Arsenal ambao wamecheza mechi 26 wataipiku Tottenham hadi nafasi ya pili wakiwa na akama 49.

Itakumbukwa kuwa Tottenham wanamechi ngumu ya kukata na shoka dhidi ya Manchester City

Kona kuelekea lango la Leicester

32' Arsenal 0-0 Leicester

LOOOOOOOOO

Olivier Giroud anafunga bao lakini refarii anakataa anasema ameotea

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Olivier Giroud

26' Olivier Giroud (Arsenal) anakosa pasi safi kutoka kwa Alex Oxlade-Chamberlain

26' Freekick

Riyad Mahrez (Leicester City)

25' Arsenal 0-0 Leicester

Kona ya , Arsenal.

Wes Morgan ameutoa nje mpira .

19'Offside Arsenal.

Olivier Giroud anachonga pasi muruwa lakini Mesut Özil ameotea

15' Je ameunawa ?

Alexis Sánchez (Arsenal) anadai Handbol lakini refarii anapuzilia mbali.

00:14 Arsenal 0-0 Leicester

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mesut Ozil

Shinji Okazaki anapoteza nafasi pia katika lango la Arsenal akiwa amesalia na kipa Peter Cech

LOOOOO

Olivier Giroud (Arsenal) anapoteza nafasi ya wazi akiwa amesalia na kipa pekee yake.

00:12 Kona- Arsenal. Danny Simpson ameutoa nje.

00:08' Olivier Giroud (Arsenal) anacheza visivyo.

00:07 Arsenal 0-0 Leicester

Udhibiti wa mpira

Arsenal 72 %-28 %Leicester4. Riyad Mahrez ameifungia Leicester mabao 14 na kusaidia katika mabao mengine 10.
Haki miliki ya picha Getty
Image caption Riyad Mahrez ameifungia Leicester mabao 14

Yeye ndiye mchezaji wa kwanza kutimiza zaidi ya mabao kumi msimu huu.

00:03

Haki miliki ya picha PA
Image caption Alex Sanchez
Sanchez anakosa mkwaju wa kichwa na inakuwa ni Golkick kuelekea lango la Arsenal. LAAAAAAAAAKona kuelekea lango la LeicesterArsenal 0-0 Leicester (3:00 EAT) 00:01Mpira umeanza kwa kasi kubwa Arsenal wanafanya mashambulizi katika lango la Leicester Wachezaji wameingia uwanjani
Image caption Arsenal 0-0 Leicester
3.Iwapo Leicester watainyuka Arsenal watafungua pengo la alama 7 na itakuwa vigumu kwa timu yeyote kuwapokonya taji msimu huu. #Arslei

Mlinzi Per Mertesacker na kiungo Francis Coquelin wanarejea kikosini .

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mlinzi Per Mertesacker na kiungo Francis Coquelin wanarejea kikosini .
Danny Welbeck anarejea baada ya kuwa nje kwa kipindi kirefu mno takriban mwaka mmoja.Mara ya mwisho alipocheza ilikuwa ni Aprili 2015.Hii itakuwa mechi ya 100 kwa mchezaji Alex Ox-Chamberlain @Alex_OxChamboArsene Wenger amefanya mabadiliko mawili katika kikosi chake
Haki miliki ya picha PA
Image caption Danny Welbeck anarejea baada ya kuwa nje kwa kipindi kirefu mno
Arsenal v Leicester (3:00 EAT)Timu ya Arsenal : Cech, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Ramsey, Oxlade-Chamberlain, Ozil, Sanchez, Giroud.

Leicester haijafanya mabadiliko yeyote kutoka kwa kile kikosi kilichoilaza Manchester City juma lililopita.

2.Kocha wa Leicester Claudio Ranieri amekihifadhi kikosi kilekile kwa mechi 6 sasa.
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Arsene Wenger

Je Kocha Arsene Wenger atakuwa kocha wa kwanza kuwazima Leicester ugeninini ?

  1. Leicester hawajapoteza hata mechi moja katika 16 walizocheza ugenini.
Timu ya Leicester : Schmeichel, Simpson, Morgan (N), Huth, Fuchs, Mahrez, Kanté, Drinkwater, Albrighton, Okazaki, Vardy.

Mechi zitakazochezwa leo Jumapili baina ya timu 4 za kwanza zitaamua mwelekeo halisi wa ligi hii yenye wapenzi wengi duniani, Ligi Kuu ya Uingereza.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Arsenal itamenyana na Leicester City

Arsenal itamenyana na Leicester City ambayo bado inaongoza ligi ikiizidi Arsenal alama 5.

Ushindi wa the Gunners utapunguza pengo baina yake na Leicester na kuipa matumaini zaidi ya kuendelea kupigana hadi mwisho.

Nayo Manchester City yenye nafasi ya 4 itaialika Tottenham iliyo kwenye nafasi ya pili.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Arsenal imo kwenye nafasi ya tatu.
Jumapili tarehe 14 Februari
  1. Arsenal v Leicester 15:00
  2. Aston Villa v Liverpool 17:05
  3. Man City v Tottenham 19:15