Barcelona yainyuka Celta De vigo

Haki miliki ya picha AP

Timu ya soka ya Barcelona jana ilifanikiwa kuinyuka Celta De Vigo kwa mabao 6-1, katika mwendelezo wa Ligi kuu ya Hispania kupitia mabao ambayo yalifungwa na wachezaji Lionel Messi ,Luis Suárez mabao , Ivan Rakitic pamoja na Neymar Neymar da Silva Santos Júnior, mchezaji Lionel Messi akifunga Hat-trick katika mchezo huo.

Mbali na mchezo huo michezo mingine Getafe iliambulia kichapo cha bao 1 – 0 kutoka kwa Atl Madrid, Real Sociedad wao walichomoza na ushindi wa mabao 3 – 0 dhidi ya Granada CF,na Sevilla ilichapa bao 2 – 0 Las Palmas.

Kwa matokeo hayo Barcelona inaongoza ligi ikiwa na pointi 57,ikifuatiwa na Altetico Madrid kwa pointi 54,nafasi ya tatu ni Real Madrid yenye pointi 53,Villarreal ipo nafasi ya Nne na nafasi ya tano ni sevilla ikiwa na pointi 40.