PSG kuwakabili Chelsea Uefa

Haki miliki ya picha AFP

Michuano ya klabu bingwa barani Ulaya itaendelea tena Jumanne usiku kwa mechi 2 za kwanza za Raundi ya Mtoano ya timu 16

Benfica ya ya Ureno itakuwa nyumbani dhidi ya Zenit Saint Petersburg na Paris St Germain (PSG) itakuwa nyumbani jijini Paris Ufaransa kuwavaa Mabingwa wa England Chelsea.

Na Jumatano, zitapigwa mechi ambapo Klabu ya KAA Gent ya ubelgiji watakuwa Nyumbani kucheza na Wajerumani VfL Wolfsburg, huku AS Roma ya Italia wakiwa nyumbani kupambana na Vigogo wa Spain Real Madrid.