Simba yasubiri mgao wa Mbwana Samatta

Haki miliki ya picha Samatta Twitter

Klabu ya Soka ya Simba nchini Tanzania iko katika mazungumzo yanayoendelea vema ili iweze kupata mgao wake baada ya aliyekuwa mchezaji wake Mbwana Ally Samatta kuuzwa huko Ubeligiji.

Simba ambayo ilimuuza Samatta klabu ya TP Mazembe mwaka 2012, inapaswa kupata asilimia 20 ya fedha ambazo TP Mazembe imelipwa baada ya kumuuza Samatta kwenye klabu hiyo ya Ubelgiji.

TP Mazembe ilimuuza Mtanzania huyo kwa Samatta KRC dola za Kimarekani 800,000