Chelsea walazwa na PSG ligi ya mabingwa

Ibrahimovic Haki miliki ya picha AP
Image caption Ibrahimovic alitangulia kufunga dakika ya 39

Klabu ya PSG kutoka Ufaransa imepata ushindi dhidi ya Chelsea mechi ya mkondo wa kwanza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya huku Benfica nao wakilaza Zenit St-Petersburg.

Chelsea wamecharazwa 2-1 ugenini Paris.

Paris St-Germain walichukua uongozi kupitia mshambuliaji matata wa Sweden Zlatan Ibrahimovic dakika ya 39.

Chelsea walisawazisha katika dakika ya 45 kupitia kwa Mikel Obi lakini Edison Cavan akaitumia dakika ya 78 kuwaumiza Chelsea.

Bao hilo la Mikel ndilo lake la sita kufungia Chelsea katika karibu miaka 10 aliyokaa katika klabu hiyo ya Uingereza.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Benfica wakishangilia ushindi

Bao pekee la Benfica, waliokuwa nyumbani, lilifungwa na Jonas muda wa ziada kutokana na mkwaju wa adhabu uliopigwa na Nicolas Gaitan.

Hilo ndilo bao lake la 25 msimu huu na la 45 kufungia Benfica katika mechi 56 tangu alipojiunga nao akitokea Valencia mwaka 2014.

Zenit walisalia wachezaji kumi uwanjani baada ya Domenico Criscito kupewa kadi ya pili ya njano dakika ya 90.

Katika ligi Championship nchini Uingereza, Blackburn Rovers walishinda 3-0 dhidi ya Fulham nao Hull City wakatoka sare 0-0 na Brighton & Hove Albion.