Isaac Mwangi atishia kujiuzulu Kenya

Haki miliki ya picha AFP

Mkuu wa Riadha nchini Kenya amesema anataka kuachia ngazi kwa muda baada ya tuhuma kuwa aliwataka wanariadha kumhonga ili kupunguziwa kifungo kutokana na utumiaji wa dawa za kusisimua misuli.

Isaac Mwangi anakanusha tuhuma hizo na anataka kuiachia nafasi yake kwa siku 21 wakati Shirikisho la Riadha Duniani likifanya uchunguzi. "Tuhuma hizi zimenisababishia usumbufu mkubwa wa mawazo" Mwangi alisema"Ningependa jina langu lisafishwe"

Wanariadha wawili waliosimamishwa walidai Mwangi aliwataka kutoa fedha ili wapunguziwe adhabu-tuhuma ambazo Mwangi anasema hazina msingi.