Simba na Yanga kukwaana ligi kuu

Nchini Tanzania Gumzo miongoni mwa wapenzi wa Soka ni kuhusiana na Mechi kubwa ya watani wa Jadi vilabu vikongwe vya Yanga na Simba itakayofanyika mwishoni mwa juma lakini kubwa zaidi sasa linalojadiliwa ni baada ya shirikisho la Soka nchini humo kutangaza kuwa mwamuzi wa mchezo huo ni mwanamama Jonesia Rukiyaa.

Mitandao inasema mwanadada huyo ni mmoja wa marefa ambao wanasimamia sheria za uwanjani kwa hakika bila kupundisha na kwa kawaida mchezo kati ya Yanga na Simba huwa ni mchezo wenye joto la hali ya juu.