FC Midtjylland yajitetea

Haki miliki ya picha All Sport

FC Midtjylland ya Denmark wameutetea uamuzi wao wa kuwauzia Tiketi mashabiki wa Manchester United kwa pauni 71 wakisema ni suala linaloendeshwa kwa mujibu wa Soko. Bila shaka mahitaji makubwa, yanafanya bei kupanda.

Mashabiki wa United ambao pia leo Timu yao itamkosa Nahodha wao Majeruhi Wayne Rooney ambaye amefunga mabao saba katika mechi zake tisa za mwisho tayari wametengeneza mabango yenye ujumbe wa kulalamika kupinga gharama hiyo wakidai ni kubwa.

Mwezi Ogasti Mashabiki wa Southamton walilipishwa pauni 22 katika Uwanja huo huo, ligi hii hii ya Europa