Lionel Messi afunga bao la 300

Haki miliki ya picha AP

Katika Uwanja wa El Molinon Lionel Messi amekuwa mchezaji wa kwanza kufikia bao la 300 katika La Liga pale ambapo amepachika mabao mawili dhidi ya Sporting Gijon. Katika mechi hiyo ambayo Sporting wameambulia goli moja, Luis Suarez naye amepiga bao lakini pia akakosa penati.

Messi alifunga la 301 dakika ya 31, wakati lile la Luis Suarez lilikuwa dakika ya 67, huku la wenyeji likifungwa na Castro Garcia dakika ya 27. Barca sasa wako point sita kileleni.