Rooney kutocheza mechi ya Europa

Haki miliki ya picha PA
Image caption Rooney nje mechi ya Yuropa

Nahodha wa kilabu ya Manchester United Wayne Rooney hatoshiriki katika mechi ya awamu ya kwanza dhidi ya kilabu ya Denmark Midtjlland siku ya Alhamisi baada ya kuwachwa nje.

Beki Matteo Darmian pia hatoshiriki katika mechi hiyo baada ya kupata jereha la bega siku ya jumamosi dhidi ya Sunderland.

Donald Love ,ambaye alicheza kwa mara ya kwanza katika mechi dhidi ya Sunderland ameorodheshwa katika kikosi hicho.

Vijana waliojiunga na timu kuu katika mechi hiyo Regan Poole ,Joe Riley na James Weir pia wameorodheshwa katika kikosi cha mechi hiyo.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Van Gaal

Rooney amefunga mabao saba katika mechi zake tisa za mwisho lakini hakuonekana katika ndege ilokuwa ikielekea Scandinavia.

Mkufunzi Louis Van Gaal anatarajiwa kuelezea kutokuwepo kwa Rooney katika mkutano na wanahabari siku ya jumatano.