Riadha: Kenya kukabiliwa na marufuku

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanariadha wa Kenya

Rais wa shirikisho la riadha duniani IAAF Lord Coe amesema yuko tayari kuwapiga marufuku wanariadha wa Kenya kutoshiriki katika michezo ya Olimpiki iwapo shirikisho la riadha nchini Kenya AK litashindwa kuafikia mahitaji ya shirika linalokabiliana na dawa za kulevya miongoni mwa wanariadha Wada.

Wiki iliopita Kenya ilishindwa kuthibitisha kwa Wada kwamba inakabiliana na udanganyifu katika riadha.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais wa IAAF Lord Sebastina Coe

Hatua hiyo inajiri wakati ambapo wanariadha kadhaa wa Kenya wamepatikana na dawa za kusisimua misuli pamoja na kuwepo kwa madai ya ufisadi.

''Lazima tuwe makini ,''alisema Coe,rais wa shirikisho la riadha duniani IAAF.Coe amesema kuwa ataliwekea taifa lolote litakalopatikana na hatia ya kutetea utumizi wa dawa hizo vikwazo vikali.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wanariadha wa Kenya

Kenya inatarajiwa kuorodheshwa miongoni mwa mataifa yanayomulikwa kwa kushindwa kuafikia mahitaji hayo ya Wada na huenda ikapigwa marufuku kushiriki katika mashindano ya kimataifa kama ilivyokuwa na wanariadha wa Urusi.