Pellegrini:Ulaya ni muhimu kuliko FA

Image caption Pellegrini

Manchester City imesema kuwa italipatia kipau mbele kombe la vilabu bingwa Ulaya badala ya mechi ya raundi ya tano ya FA dhidi ya Chelsea siku ya jumapili huko Stamford Bridge,kulingana na kocha Manuel Pellegrini.

City itacheza awamu ya kwanza ya kombe la vilabu bingwa Ulaya huko Dynamo Kiev siku ya jumatano,ikiwa ni siku nne kabla kucheza fainali ya kombe la Capitol One.

Raia huyo wa Chile amesema:Lengo letu ni mechi inayofuata lakini lazima tuangazie kilicho muhimu kwa sasa kutokana na mejeraha mengi.

City itakaribishwa ugenini na Chelsea siku ya jumapili.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Pellegrini

Washindi hao wa kombe la FA mwaka 2011 bado wanapigania kushinda mataji matatu ikiwemo lile la Ligi,Kombe la Ligi na lile la vilabu bingwa Ulaya.

Watalazimika kucheza mechi katika mashindano yote katika kipindi cha siku 11 kati ya Februari 21 na Machi 2.