Nadal ashindwa kwa Cuevas

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rafael Nadal apoteza mchzo mbele ya Pablo Cuevas

Mcheza Tenisi Rafael Nadal jana alishindwa kutinga katika hatua ya Nusu Fainali ya mashindano ya Tenisi ya ATP baada ya kupoteza mchezo kwa seti tatu kwa Mruguay Pablo Cuevas katika mashindano ya wazi ya Rio .

Mshindi huyo wa mara 14 wa Grand Slam alianza kwa kuongoza kwa pointi mbili kwa seti mbili lakini baadaye alianza kupoteza mchezo kwa kufungwa jumla ya 6-7 (6) 7-6 (3) 6-4.

Pamoja na kupoteza mchezo huo Nadal amesema amekubali kushindwa na atajaribu kulifanyia kazi na kubadili mwelekeo.

Cuevas ambaye anashikilia nafasi ya 45 ulimwenguni atakutana na Guido Pella katika hatua ya fainali.