Man Utd kushuka dimbani Kombe la FA

Man Haki miliki ya picha PA
Image caption Manchester United wameshindwa mechi mbili za karibuni zaidi

Manchester United watashuka dimbani leo dhidi ya katika raundi ya tano ya Kombe la FA wakijaribu kuandikisha matokeo mazuri baada ya kushindwa mechi mbili za majuzi zaidi.

Watakuwa ugenini Greenhous Meadow dhidi ya Shrewsbury Town saa tano kasorobo saa za Afrika Mashariki.

United wanatarajiwa kuwa bila kipa wao David de Gea aliyeumia goti kabla ya mechi ya Europa League ambayo walishindwa 2-1 na FC Midtjylland nchini Denmark.

Kabla ya kushindwa na klabu hiyo ya Denmark, walikuwa wamelazwa 2-1 na Sunderland Ligi ya Premia.

De Gea ndiye mchezaji wa 14 wa United kuumia, miongoni mwao akiwa nahodha Wayne Rooney.

Kiungo wa zamani wa Manchester United anayechezea Shrewsbury Larnell Cole atarejea kikosini baada ya kukosa mechi tatu kutokana na jeraha.

Meneja Micky Mellon pia amethibitisha kwamba difenda Jack Grimmer yuko sawa kucheza.

Mshindi wa mechi hii atakutana na West Ham United katika robo fainali.