Manchester united yaiadhibu Shrewsbury

Haki miliki ya picha Getty

Klabu ya Manchester united jana ilifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya FA baada ya kuvuna ushindi mnono dhidi ya Shrew-Sbury Town wa mabao 3-0.

Mabao ya Manchester united yamefungwa kupitia wachezaji wake Chris Smalling , Juan Mata na Jesse Lingard .

Baada ya ushindi huo sasa Manchester united itakutana na West Ham United katika hatua ya robo fainali Mechi ambazo zinatarajia kuchezwa wikiendi ya Machi 11 na 14 mwaka huu.

Chelsea itamenyana na Everton katika mchezo wa Robo Fainali baada ya kuiondoa Manchester City, Crystal Palace wakiongozwa na wao watasafiri kuikabili Reading , Watford watakuwa wageni kati ya Arsenal au Hull