Arsenal kuikabili Barcelona UEFA

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kikosi cha Arsenal kikifanya mazoezi kujiandaa dhidi ya Barcelona

Arsenal leo wanatarajiwa kuwa wenyeji wa Barcelona katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora kesho kabla ya kurudiana nao tena Camp Nou Machi 16 mwaka huu.

Barcelona wanapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo lakini Henry anaamini Arsenal wanaweza kuwa na nafasi kama meneja wake Arsene Wenger akibadilisha mbinu zake.

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry amedai kuwa timu hiyo inapaswa kutumia mipira ya kushtukiza na kuepuka kukaa na mipira kama wanataka kuwa na nafasi ya kuifunga Barcelona.

Katika makala yake aliyoandika kuhusiana na mchezo huo, Henry amedai Arsenal wanapaswa kukubali kuwa hawatakuwa na nafasi ya kumiliki mpira kwa kipindi kirefu kama walivyozoea na pindi wanapopata nafasi wanapaswa kuitumia ipasavyo.

Henry amesema ni mara chache timu inaweza kupata nafasi ya kucheza na Barcelona hivyo Wenger anapaswa ajiandae kubadili mbinu zake za kushambulia pindi awapo nyumbani na ugenini.

Barcelona imekuwa katika kiwango bora msimu huu, wakiongoza La Liga kwa tofauti ya alama nane baada ya kuichapa Las Palmas kwa mabao 2-1 juzi.

Mchezo mwingine ni kati ya Juventus na Bayern Munich.