Apanga kukimbia marathon 27 katika siku 27

Haki miliki ya picha Sportsrelief
Image caption Mchekeshaji kutoka Uingereza Eddie Izzard

Mchekeshaji kutoka Uingereza Eddie Izzard amekamilisha marathon yake ya kwanza kati ya 27 alizopanga kukimbia ilikuchanga pesa za kuisadia shirika lisilokuwa la kiserikali la Sport Relief.

msanii huyo amepanga kukimbia mbio 27 katika siku 27 kila mmoja ikiashiria mwaka aliofungwa jela kiongozi wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini hayati mzee Nelson Mandela.

"mbio za kwanza 10 ndizo huwa ngumu zaidi lakini baada ya hapo inakuwa rahisi tu kwani mwili na akili tayari huwa umekubali'' alisema Izzard.

Hii si mara ya kwanza kwa Izzard kujaribu kushiriki katika msururu wa mbio za marathon.

Mwaka wa 2012 Izzard alijaribu kukimbia wakati huo akiwa Afrika Kusini., hata hivyo hakumaliza.

mwili wake ulishindwa kustahimili kushiriki mbio nyingi hivyo kwa wakati mmoja.

''nikiulizwa kwanini nafanya hivi, huwa ninajibu kuwa nafkiri kuna watu ambao wamefanya mambo ya ajabu zaidi ''

Izzard mwenye umri wa miaka 54 alichapisha picha moja akiwa milimani karibu na mto Mbashe ulioko kwenye jimbo la Eastern Cape.

Kisha saa chache baadaye akarusha picha nyengine akisema kuwa amekimbia maili 16 (kilomita 25)

Haki miliki ya picha Izzard Sportsrelief
Image caption Je ataweza kumaliza marathon 27 katika siku 27 ?

Vilevile alionekana akivuta pumzi huku mtu akimkanda kanda miguu yake.

Hatimaye, nimemaliza marathon yangu ya kwanza'' alisema bwana Izzard.

Kila marathon inaurefu wa kilomita 42.

Je ataweza kumaliza marathon 27 katika siku 27 ?

Tuma majibu yako kwenye ukurasa wetu wa facebook tafuta BBCSwahili.