Mchezaji aliyempa refa ''kadi nyekundu'' apongezwa

Image caption Trabzonspor

Mashabiki wa kilabu Trabzonspor wamefanya maandamano wakimuunga mkono mchezaji mmoja ambaye alipewa kadi nyekundu kwa kumuonyesha kadi nyekundi refa.

Salih Dursun alibeba kadi nyekundu na kumuonyesha refa Deniz Bitnel na kuwa mchezaji wa nne wa Trabzonspor kutolewa nje katika mbapo kilabu hiyo ilishindwa 2-1 na Galatasaray.

Hatahivyo,amepata ufuasi kwa hatua yake,huku Bitnel akikosolewa kwa mchezo wake.

Trabzonspor pia imeanza kuuza fulana zinazomuonyesha Dursun akifanya kitendo hicho.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mchezaji Dursun ampatia refa kadi nyekundu

Kumekuwa na ripoti kwamba maafisa wa kilabu hiyo huko Macka wanapanga kujenga sanamu ya mchezaji huyo ili kuunga mkono kitendo chake.

Na huku mashabiki wa kilabu hiyo wakibeba kadi nyekundu wakiandamana huko Trabzon,mashabiki katika jimbo la magharibi la Koceli wamewasilisha malalamishi ya uhalifu kwa utumizi m'baya wa mamlaka na kuchochea chuki.

Tranzospor walikuwa chini na wachezaji tisa huku ikiwa mabao ni 1-1 wakati refa Bitnel alipompatia kadi nyekundu Luis Cavandi kwa kucheza visivyo mbali na kuizawadi Galatasaray mkwaju wa penalti.

Image caption Mchezaji wa kilabu ya Trabzonspor

Wakati wa maandamano hayo dhidi ya refa uwanjani,kadi hiyo nyekundu ilianguka kabla ya Dursun kuiokota na kumuonyesha refa,ambaye alimpokonya mchezaji huyo na kumuonyesha vilevile hatua iliosababisha mchezaji huyo kuondoka uwanjani.