Djokovic ajiondoa kwenye Mashindano

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Novak Djokovic ajiondoa baada ya kuumwa jicho

Mchezaji Tenisi Novak Djokovic alilazimika kujiondoa kwenye mashindano ya tenisi ya Dubai hatua ya robo fainali katika mchezo dhidi ya Feliciano Lopez.

Mchezaji huyo namba moja wa Tenisi Duniani anasumbuliwa na tatizo la jicho na amejiondoa baada ya kupoteza seti ya kwanza (6-3).

Mhispania Lopez sasa atakutana na Cypriot Marcos katika hatua ya nusu fainali na Djokovic mpaka sasa ameshinda michuano ya Dubai mara nne .

Djokovic mwenye umri wa miaka 28 alionekana akimuita kocha wake wakati wa mchezo na kumwambia tatizo la kusumbuliwa na jicho kabla ya kumaliza mchezo .