Sexwale ajiondoa uchaguzi wa urais FIFA

Sexwale Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bw Sexwale alikuwa mgombea pekee kutoka Afrika

Mgombea wa urais wa Fifa kutoka Afrika Tokyo Sexwale kutoka Afrika Kusini amejiondoa kutoka kwenye uchaguzi wa kuchagua mrithi wa Sepp Blatter.

Bw Sexwale, akihutubu kabla ya kura kupigwa, amesema hataki kugawanya kura na akawahimiza wajumbe waamue kati ya wagombea wane waliosalia.

Ameahidi kuunga mkono na kufanya kazi na atakayeshinda.

"Nafikisha kampeni yangu kikomo hapa," amesema.

Wagombea waliosalia ni Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa, Gianni Infantino, Mwana mfalme Ali bin al-Hussein, na Jerome Champagne.