Ox-lade Chamberlain nje na Jeraha

Image caption Alex Chamberlain kuuguza jaraha kwa wiki kadhaa

Kiungo wa kati wa kilabu ya Arsenal Alex Oxlade Chamberlain hatocheza kwa wiki kadhaa kutokana na jeraha la goti ,mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alipata jeraha walipokabiliana na Javier Mascherano wakati wa mechi ya Jumanne ya vilabu bingwa Ulaya.

Aliondoka katika uwanja wa Emirates akiwa na magongo.

''Tulimpoteza Chamberlain siku ya jumanne.Jereha lake ni baya na litamuweka nje kwa wiki kadhaa,''alisema Wenger.