Wapenzi wa FIFA 2016 wataka Rashfold atuzwe

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Wapenzi wa FIFA2016 wataka Rashfold atuzwe

Watumiaji wa programu za michezo ya kielektroniki wanawataka watengenezaji wa mchezo wa FIFA 2016 kuimarisha hadhi ya mchezaji chipukizi wa Manchester United , Marcus Rashford.

Shinikizo hilo linafuatia mwanzo wenye ufanisi mkubwa katika mechi zake za ligi kuu ya uropa na ile ya uingereza dhidi ya Arsenal ambapo kijana huyo alifunga mabao mawili.

Kulingana nao mchezaji huyo aliyefufua matumaini ya Manchester United msimu huu anapaswa kutambuliwa na kupewa hadhi ya juu anayostahili katika programu hiyo ya FIFA 2016.

Kocha wa Man United Louis Van Gaal alimsifu kwa ''kipaji chake cha kipekee''.

Hata kocha wa timu hasimu Arsenal, Arsene Wenger alitamaushwa na uwezo na uweledi wa chipukizi huyo machachari aliyefuma mabao mawili ya kwanza dhidi yao siku ya jumapili.

Sasa mashabiki wake wanataka kampuni inayoitengeneza programu hiyo waimarishe hadhi yake.

Kampuni hiyo ya EA Sports, huwa inamuorodhesha mchezaji yeyote na kutathmini ubora wake na kumpa alama juu ya 100% ima ni ushambuliaji kasi na uwezo wake wa kufunga mabao.

Katika programu hiyo kwa sasa Rashford amepewa hadhi ya mchezaji wastani na jumla ya alama 59 (ambayo sio nzuri ya kutosha kwa mujibu wa wafuasi wa klabu hicho cha Manchester United).

Aidha Rashford anagharimu takriban pauni laki tatu pekee (300,000) katika soko hilo la kielektroniki ambalo huendeshwa kwa njia sawa na soko la wachezaji wa ligi kuu ya Uingereza.

Mmiliki mmoja wa programu hiyo ya FIFA 2016 ernie_els alichapisha hoja kwenye mitandao akidai kuwa ''Rashford ndiye mshambuliaji nyota katika ligi kuu ya Uingereza kwa sasa'' Aidha alimfananisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 na Ronaldo na kumbatiza jina "Rashaldo".

Vilevile EA Sports walishauriwa moja kwa moja : "Kufanya lisilobudi yaani,kuimarisha hadhi yake kulingana na matokeo yake uwanjani kwa kumpa alama za juu zaidi takriban asilimia 65% jumla na asilimia 70% katika ushambuliaji na umahiri wake.

Haki miliki ya picha GETTY
Image caption Rashford anagharimu takriban pauni laki tatu pekee (300,000) katika soko hilo la kielektroniki

''Aidha kasi yake ikitathminiwa kuwa kati ya 77-78% huku ubora wake ukikisiwa kupanda hadi kati ya asili mia 82-83''.

Mikey Kalinowski naye alisema kuwa ''kwa kweli ni mapema mno kumsawazisha na kigogo wa soka ya Argentina na Barcelona ya Uhispania Lionel Messi.

Hata hivyo aliendelea kusema kuwa Rashford ni mbora kumzidi Messi''

Hayo yote ni kenda mpenzi msomaji tuachie maoni yako kuhusu ripoti hii kupitia mitandao yetu ya kijamii katika Facebook Twitter na Instagram tafuta BBCSwahili.