Petr Cech kuwa nje wiki tatu Arsenal

Cech Haki miliki ya picha PA
Image caption Cech aliumia wakati wa mechi dhidi ya Swansea

Arsenal watamkosa mlinda lango wao Petr Cech kwa wiki tatu hadi wiki nne kutokana na jeraha, meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger amesema.

Kipa huyo wa umri wa miaka 33 atakosa mechi tatu za Ligi ya Premia, pamoja na mechi muhimu ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ugenini dhidi ya Barcelona.

Aidha, atakosa mechi ya marudiano Kombe la FA dhidi ya Hull.

Aliumia mguuni alipokimbia kurejea kwenye ngome yake baada ya kuruka juu kudaka mpira wa kona wakati wa mechi ya Jumatano ambayo walichapwa 2-1 na Swansea nyumbani.

The Gunners wamo nambari tatu ligini, alama sita nyuma ya viongozi Leicester, na alama tatu nyuma ya Tottenham walio nambari mbili.

Arsenal, wanaojaribu kushinda taji la Ligi ya Premia mara ya kwanza tangu 2004, watakuwa ugenini dhidi ya Spurs Jumamosi.

Tarehe Wapinzani Michuano

Jumamosi, 5 Machi Tottenham (Ugenini) Ligi ya Premia

Jumanne, 8 Machi Hull (Ugenini) Marudiano (Kombe la FA)

Jumamosi, 12 Machi West Brom (Nyumbani) Ligi ya Premia

Jumatano, 16 Machi Barcelona (Ugenini) Champions League last 16

Jumamosi, 19 Machi Everton (Ugenini) Ligi ya Premia

Jumamosi, 2 Aprili Watford (Nyumbani) Ligi ya Premia