FIFA:Sheria ya kanda za video kuangaliwa kujaribiwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Shirikisho la soka duniani FIFA

Bodi ya shirikisho la soka ya kimataifa imeidhinisha majaribio ya kanda za video zitakazochezwa kwa mara nyengine ili kuwasaidia maafisa wa mechi kufanya uamuzi mzuri.

Teknolojia hiyo itajaribiwa katika mechi kadhaa katika kipindi cha miaka miwili.

Utumizi wa kanda za video kuchezwa tena kutaachiwa marefa kutoa uamuzi wa iwapo bao limefungwa,penalti inafaa kutolewa ama iwapo mchezaji anafaa kupewa kadi nyekundu ama kwa makosa ya utambuzi wa wachezaji.

Rais wa FIFA Gianni Infantino ameilezea sheria hiyo kama ya kihistoria katika soka.

Amesema kuwa mchezo huo umeonyesha kwamba unawasikiza wachezaji na mashabiki.