Yanga kuwakabili African Sport

Image caption Kikosi cha Yanga ya Tanzania.

Ligi kuu ya Tanzania bara itaendelea tena leo kwa mchezo mmoja kuchezwa katika uwanja wa taifa Jijini Dar es Salaam.

Klabu ya Yanga watakuwa wenyeji wa wana Kimanumanu African Sports, mchezo utakaopigwa katika dimba la taifa jijini Dar es salaam, mchezo utakaochezwa saa 10:30 kwa saa za Afrika Mashariki. Yanga wako katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi wakiwa na alama 47 wakiwa wamecheza michezo 20 nyumba ya wapinzani wao Simba walioko kileleni kwa alama 48 wakiwa wamecheza michezo 21. Kikosi hicho cha wanajangwani kimeshinda michezo 14, na kwenda sare michezo mitano huku kikipoteza mchezo mmoja. African sport wao wako katika nafasi ya 15 nafasi moja toka mwisho wakiwa wamecheza michezo 21 wana alama 17.