Hull City kuchuana na Arsenal FA

Haki miliki ya picha PA
Image caption Arsenal dhidi ya Hull City

Hull City na Arsenal zinatarajiwa kufanya mabadiliko makubwa katika vikosi vyao vya kwanza vitakavyokutana katika mechi ya marudiano ya kombe la FA siku ya jumanne.

Arsenal watasafiri hadi Hull kufuatia sare ya 0-0 katika mechi ya kwanza iliochezwa katika uwanja wa Emirates.

Hull City ina kikosi kizima cha kuchagua ,huku Shaun Maloney na Nick Powell wakitarajiwa kuanza.

Petr Cech na Laurent Kolscieny wote wanauguza majeraha ya miguu na hawatashiriki katika mechi hiyo muhimu huku Francis Coquelin akihudumia marufuku.

Wanajiunga na Jack Wilshere,aliye na jeraha la mguu,Tomas Rosicky aliye na jeraha la paja na santi Carzola mwenye jeraha la mguu, Alex Oxlaide Chamberlain mwenye jeraha la mguu pia hatocheza katika mechi hiyo.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wachezaji wa Hull City

Arsenal ambayo inajaribu kubeba kombe la FA kwa mara ya tatu msimu huu,hawajashinda katika mechi tano za michuano yote,huku Hull wakiwa katika nafasi ya tatu ya ligi ya daraja la kwanza baada ya kushinda mechi moja kati ya tano walizocheza.

Washindi wa mechi hiyo watakabiliana na Watford katika robo fainali ya kombe hilo.