Chelsea yalazwa na PSG

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Chelsea dhidi ya PSG

Matumaini ya Chelsea katika kombe la vilabu bingwa Ulaya yaliangamizwa na kilabu ya PSG katika mechi ya mchujo wa kufuzu robo fainali huku mshambuliaji wa PSG Zlatan Ibrahamovich akiiongoza timu yake kupata ushindi katika uwanja wa Stamford Bridge.

PSG iliimarisha uongozi wao wa 2-1 kutoka mechi ya awamu ya kwanza baada ya Ibrahimovic kumuandalia krosi safi Adrien rabiot aliyefunga akiwa karibu na goli baada ya dakika 16.

Diego Coast hatahivyo alisawazisha kabla ya muda wa mapumziko lakini baada ya kutolewa na jeraha Ibrahimovic alifunga bao la pili kupitia pasi muruwa ya Angeli di Maria iliisaidia PSG kufika robo fainali ya kombe hilo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Chelsea dhidi ya PSG

Wageni hao ambao waliiondoa Chelsea kutokana na sheria ya bao la ugenini ,walimaliza usiku huo kwa kutawala mechi yote.

Chelsea ambayo ipo katika nafasi ya 10 katika jedwali la ligi ya Uingereza sasa inakabiliwa na tishio la kutoshiriki katika ligi ya bara Ulaya msimu ujao,huku Costa na Eden Hazard wakitolewa katika mechi hiyo na jeraha kabla ya mechi ya robo fainali ya FA dhidi ya Everton.