Matokeo ya ligi kuu Tanzania

Image caption ligi kuu Tanzania

Ligi kuu ya Tanzania bara iliendelea siku ya Jumatano kwa michezo minne kupigwa

katika dimba la Mkwakwani mkoani Tanga , Coastal Union waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mgambo Jkt.

Tanzania Prison wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Sokoine walitoshana nguvu na Kagera Sugar kwa kufungana bao 1-1.

Nao Mwadui Fc wakikipiga na Majimaji wametoshana nguvu kwa sululu ya 0-0,JKT Ruvu wakawachapa Toto African kwa mabao 2-0.

Ligi hiyo itaendelea tena hapo kesho kwa Simba kucheza na Ndanda FC,Mbeya City watawaalika Staind United, katika dimba la Sokoine.