Mshambuliaji wa Kenya anayechezea Ulaya asifiwa

Image caption Olunga

Kocha wa timu ya IF Djurgarden Per Pelle Olsson amemsifu aliyekuwa mshambuliaji wa kilabu ya Gor Mahia Michael Olunga baada ya kufunga bao jingine katika mechi ya kirafiki iliochezwa siku ya ijumaa.

Olunga alifunga bao katika kipindi cha kwanza cha mchezo lakini bao hilo halikutosha kwani Djurgaden walitoka sare ya 2-2 dhidi ya Elfsborg.

Akizungumza baada kipenga cha mwisho, mkufunzi wa klabu hiyo Olsson alimsifu mchezaji huyo wa zamani wa K'Ogalo akimtaja kuwa mshambuliaji kamili.

''Olunga ni mchezaji mzuri sana.Pia anaonyesha kwamba ana uwezo wa kusoma mechi.Ni mchezaji mwenye kasi licha ya ukubwa wake,kwa hivyo kwa jumla atatusaidia sana kwa upande wetu''.