Sharapova 'kujisafishia jina'

Haki miliki ya picha AP
Image caption Sharapova

Mchezaji nyota wa tenisi Maria Sharapova amesema kuwa yuko tayari kujisafisha jina baada ya kupatikana na dawa za kusisimua misuli.

Katika mtandao wake wa facebook ambapo amekosoa ripoti potofu na zilizoongezwa chumvi,raia huyo wa Urusi amekana kutumia dawa ya Meldonium kila siku mbali na kupuuza onyo alilopewa mara tano kwamba angepigwa marufuku.

Pia alikosoa utawala wa mchezo huo kwa kuficha habari hiyo.

Sharapova mwenye umri wa miaka 28 atapigwa marufuku kwa mda kuanzia Machi 12.

Bingwa huyo mara tano wa Grand Slam ambaye anakabiliwa na marufuku ya hadi miaka minne amesema amekuwa akitumia dawa hiyo ambayo sasa imeorodheshwa katika shirika la kukabiliana na dawa za kusisimua misuli michezoni kwa sababu za kiafya.