Ligi Kuu ya Tanzania kuendelea leo

Ligi Kuu ya Tanzania inatarajiwa kuendelea leo kwa mchezo mmoja, ambapo Azam FC watawakaribisha Stand United.

Ijumaa mkoani Shinyanga katika uwanja wa Kambarage, wakata miwa wa Kagera Sugar watakua wenyeji wa ndugu zao kutoka wakata miwa Mtibwa Sugar kutoka Manungu Turiani.

Wikiendi Jumamosi na Jumapili ligi hiyo itaendelea kwa michezo mitano kuchezwa katikwa viwanja mbalimbali nchini, jijini Tanga wenyeji Coastal Union wakiwa wenyeji wa Simba SC katika uwanja wa Mkwakwani jijini humo.

Majimaji FC itakua nyumbani katika uwanja wa Majimaji mjini Songea kucheza na Mbeya City, huku chama la wana Stand United wakiwakaribisha Ndanda FC katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.