Barcelona yaibamiza Arsenal Uefa

Haki miliki ya picha AFP

Barcelona imetinga hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa ulaya baada ya kuifumua Arsenal 3-1 usiku wa Jumatano.

Mabao ya Barcelona yalifungwa na wachezaji Neymar da Silva Santos, Luis Suarez na Lionel Messi akahitimisha idadi ya mabao hayo dakika ya 88.

Na goli pekee la kufutia machozi la Arsenal limefungwa na Mohamed Elneny dakika ya 51 kipindi cha pili.

Barcelona imeifunga Arsenal jumla ya mabao 5-1 kufuatia ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa dimba la Emirates.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Neymar akifungia Barcelona uwanjani Nou Camp

Katika mwingine Bayern Munich imechomoza na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Juventus ya Italia.

Mabao ya Bayern yamefungwa na Lewandowski, Thomas Muller, Thiago Alcantara na Kingsley Coman, huku magoli ya Juventus ya kifungwa na Paul Pogba, na Juan Cuadrado.

Kwa matokeo hayo Bayern imeshinda jumla ya bao 6-4 kufuatia sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa awali.