Rousseff ajitetea

Haki miliki ya picha Getty

Rais wa Brazil Dilma Rousseff ametetea uamuzi wake wa kumteua mtangulizi wake Rais wa zamani wa Brazil, kuwa mkuu wa ofisi yake.

Bi Rousseff amesema kuwa kiongozi huyo wa zamani Luiz Inacio Lula da silva ana ujuzi mkubwa wa kisiasa na hivyo atasaidia kukomboa uchumi wa nchi uliokuwa unaanguka.

Punde tu baada ya uteuzi huo, wanaharakati nchini Brazil walikusanyika nje ya Ikulu ya nchi hiyo na kutumia vipaza sauti huku wakimtaka Rais Rousseff kujiuzulu kwa kuwa uteuzi wake ni miongoni mwa njama za kukwepa uchunguzi wa ufisadi unaondelea.

Rousseff amekana kwamba kuchaguliwa kwa Lula da Silva ni sehemu ya mkakati wa kumkinga Rais mstaafu kuchunguzwa kuhusiana na rushwa.

Madai ambayo Rousseff ameyakana.

Rousseff amesema Lula ni mwanasiasa mwenye ujuzi na ni kiongozi mwenye uzoefu mkubwa ambae atasaidia kuimarika kwa hali ya uchumi.

Katika muda wa miaka nane ambayo Lula alikuwa madarakani, uchumi wa Brazil uliimarika.