Johanna Konta atupwa nje BNP Paribas

Mchezaji Tenisi namba moja wa Uingereza Johanna Konta ametupwa nje ya mashindano ya wazi ya BNP Paribas ya India baada ya kufungwa

Konta amedondoshwa na Karolina Pliskova baada ya kufungwa seti 7-6, 3-6, 6-3 na Karolina Pliskova.

Kwa upande wake Novak Djokovic ameshinda seti 7-5 mara mbili dhidi ya mjerumani Philipp Koshleiber.

Naye Rafael Nadal amemshinda Fernando Verdasco kwa seti 6-0, 7-6 ambazo ni sawa na alama (11-9) huku Serena Williams akimshinda Kateryna Bondarenko seti 6-2 6-2 na kutinga hatua ya robo fainali.