Manchester United kuvaana na Liverpool

Van Gaal Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Manchester United walichapwa 2-0 mechi ya mkondo wa kwanza

Mechi za marudiano za raundi ya mtoano ya timu 16 za Uefa Europa League zitaendelea leo Alhamisi kwa michezo minane.

Manchester United na Tottenham zote ziko viwanja vya nyumbani kwao vikidaiwa kushinda kwa ushindi wa kishindo ili kutinga Robo Fainali kufuatia vipigo katika Mechi zao za kwanza.

Tottenham, maarufu kama Spurs wako kwao White Hart Lane Jijini London kurudiana na Vigogo wa Germany Borussia Dortmund ambao walishinda Mechi ya kwanza 3-0 na hivyo Spurs wanapaswa kushinda 4-0 ili kusonga.

Nako huko Old Trafford ni marudiano ya mahasimu wakubwa wa Soka la England ambapo Man United wanatakiwa waifunge Liverpool 3-0 ili wasonge baada ya kutandikwa 2-0 Wiki iliyopita huko Anfield kwa Bao za Penati ya Daniel Sturridge na Roberto Firmino.

  • Manchester United 23:05 Liverpool

(Jumla 0-2)

  • Tottenham Spurs 23:05 Borusia Dortmund

(Jumla 0-3)

  • Bayer Leverkusen 21:00 Villarreal

(Agg 0-2)

  • Lazio 21:00 Sparta Prague

(Agg 1-1)

  • Valencia 21:00 Athletico Bilbao

(Jumla 0-1)

  • Anderlecht 23:05 Shaktar Donetsk

(Jumla 1-3)

  • Sevilla 23:05 FC Basel

(Jumla 0-0)

  • Sporting Braga 23:05 Fenerbah├že

(Jumla0-1)