Timu ya Wanawake Twiga Stars yatolewa

Image caption Kikosi cha Twiga Stars

Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania Twiga Stars imetupwa nje katika michezo ya kusaka tiketi ya kuwania kuzufu kwa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika.

Twiga imeambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji Zimbabwe ‘Mighty Warriors’ katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Rufaro jijini Harare.

Katika mchezo wa kwanza ulichezwa Jiji Dar Es Salaam Twiga Stars walichapwa kwa mabao 2-1 mchezo uliochezwa kwenye dimba la Azam Complex.

Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake zitakazofanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini Cameroon.

Kikosi hicho cha Twiga Stars kinatarajiwa kurejea nyumbani leo hii mchana.