Tenisi: Djokovic ataka wanaume walipwe zaidi

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Novak Djokovic

Mchezaji nambari moja duniani katika mchezo wa tenisi Novak Djokovic amekosoa kutolewa kwa kiasi cha fedha sawa miongoni mwa wanaume na wanawake katika mchezo huo,akisema wanaume wanafaa kulipwa zaidi kwa kuwa wana mashabiki wengi.

Baada ya kushinda taji la BNP Paribas huko India Wells,alitetea kiwango cha mashabiki kuangazia kiwango cha fedha kinachotolewa kwa wanamichezo wa jinsia zote mbili.

Awali,mkurugenzi mkuu wa mashindano ya Indian Wells Ray Moore alisema kuwa michuano ya WTA inafanikishwa kutokana na kiwango cha mashabiki wanaowashabikia wachezaji wa kiume.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Serena Williams

Djokovic aliyataja matamshi yake kama yasio sawa.

Mchezaji huyo wa Serbia alisema kuwa wanawake walipiginia walichokuwa wakitaka na wakapata,na kwamba wachezaji wanaume wanafaa kupigania haki zao zaidi.