Kenya,Tanzania uwanjani kombe la mataifa Afrika

Image caption Taifa Stars ya Tanzania imesafiri Chad kwa mechi ya kundi ya la G

Kenya, Tanzania na Sudan Kusini zitakuwa uwanjani hapo kesho kutafuta tiketi ya safari ya Gabon mwakani kwa mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika..

Kenya iko ugenini dhidi ya Guinea Bissau kundi E, Tanzania imesafiri Chad kwa mechi ya kundi ya la G huku Sudan Kusini ikiikaribisha ikiikaribisha Benin mechi ya kundi C..

Mechi zingine zitakazochezwa kesho ni Sao Tome wako nyumbani dhidi ya Libya kundi F na Zambia wanakaribisha Congo kundi E, na kesho kutwa mechi ya kundi la B, Madagascar inapambana nyumbani na Afrika ya Kati..

Harambee Stars ya Kenya itakuwa na wachezaji wake wa kutegemewa wa ng'ambo wakiongozwa na kiungo mkabaji wa Southampton Victor Wanyama, kipa Arnold Origi na Michael Olunga.

Image caption Nahodha wa Kenya Victor Wanyama

Baada ya kucheza mechi mbili Kenya ni ya tatu na pointi moja tu, Congo ikiwa juu na pointi nne ikifuatiwa na Congo na Zambia..

Nahodha mpya wa Taifa Stars ya Tanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ni tegemeo kubwa kwenye mechi yao na Chad.

Taifa Stars ni ya tatu kundi G na pointi moja tu kwa mechi mbili walizocheza, kwanza wakameza mabao matatu bila jibu kisha wakaenda sare na Super Eagles ya Nigeria.

Misri inaongoza kundi hilo na pointi sita, Nigeria ya pili na nne..

Image caption Alex Iwobi wa Arsenal na Nigeria

Nigeria kwa sasa inaomba na kuamini kuwa nyota wa Arsenal Alex Iwobi atapata afueni na kuiwakilisha taifa hilo Super Eagles ya Nigeria itakapochuana na Firauni..

Sudan Kusini inashikilia nafasi ya pili kundi C na pointi tatu huku Mali ikiwa juu na nne, Benin ya tatu na Equatorial Guinea ya mwisho..

Mechi za marudiano zitachezwa wikendi hii kwa wanaocheza kesho...