Taifa Stars ya Tanzania kuikabili Chad

Image caption Taifa Stars ya Tanzania kuchuana na Chad Jumatano

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars itashuka dimbani hapo kesho, huko nchi Chad katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 11 kwa saa za nyumbani Afrika Mashariki.

Taifa Stars, imefanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo huo katika uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat Ouya ulipo katika jiji la D'jamena.

Kocha anayekinoa kikosi hicho Charles Boniface Mkwasa amesema anashukuru vijana wake hakuna majeruhi na wote wameweza kufanya mazoezi aliyoyapangilia.